
Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona Lionel Messi na baba yake wamenusurika kwenda jela baada ya kupatikana na hatia katika kesi iliyokuwa ikiwakabili ya kukwepa kulipa kodi.
Mwezi Julai mwaka jana Lioneil Messi na baba yake walikutwa na hatia katika kesi hiyo iliyokuwa ikiwakabili na baada ya hukumu waliamriwa kulipa faini au kutumikia kifungo.
Taarifa zinasema Lioneil Messi amekubali kulipa faini ya euro 252,000 na baba yake akilipa euro 180,000 na hiyo itawafanya kuepuka kifungo kilichokuwa kinawakabili.
Messi na baba yake walihukumiwa kifungo cha miaka 21 japokuwa kifungo hicho kilikuwa cha nje ya gereza kwa kuwa ilikuwa ni chini ya miaka miwili.
Post A Comment: