ads

Watu 10 wamejeruhiwa na wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa Morogoro, watatu kati yao wakiwa na hali mbaya baada ya basi la kampuni ya Karim walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori.


Walikuwa wakitoka Turiani kwenda Morogoro ndipo basi hilo lilipogongana uso kwa uso na lori lililokuwa likitokea Morogoro kwenda nchini Rwanda.

Walioshuhudia ajali hiyo walisema ilitokea jana saa sita mchana eneo la Ranchi ya Dakawa wakati dereva wa lori alipojaribu kuyapita magari mawili bila ya kuchukua tahadhari.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema majeruhi walikuwa 24 na baada ya kufikishwa hospitali wengine walitibiwa na kuruhusiwa na waliolazwa ni 10, watatu wakiwa na hali mbaya.

Alisema dereva wa lori hilo anashikiliwa na polisi.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: