ads

Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Massay amemuomba Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole kufikisha kilio cha wananchi kwa Serikali ili wapatiwe chakula cha njaa.


Massay amesema hayo leo baada ya Polepole kufanya ziara ya siku mbili wilayani Mbulu ya kukagua uhai wa chama,  kusikiliza kero na kuzungumza na Halmashauri Kuu ya CCM, Wilaya ya Mbulu.

Amesema hivi sasa wananchi wana wakati mgumu kutokana na bei kubwa ya vyakula wanavyonunua kutokana na ukame uliotokea msimu uliopita hivyo Serikali iwapatie chakula cha bei nafuu.

Amesema wananchi wa eneo hilo ni hodari kwa kulima mazao mbalimbali ya chakula na biashara, ila kutokana na ukame uliotokea msimu uliopita hivi sasa wanakabiliwa na upungufu wa chakula.

“Kwa sababu chama ndiyo kinasimamia Serikali, kilio hiki cha wananchi tunakifikisha kwako ili tatizo lao limalizike, kwani wanataka chakula cha bei nafuu na siyo kile chakula cha bure,” amesema Massay.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: