ads

Waziri mkuu wa Zamani Edward  Lowassa  amewaahidi wafuasi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema pamoja na wale wa umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu utakaofanyikaoktoba 25 mwaka 2015.

Lowassa alisema hayo jana mara baada ya kukabidhiwa fomu ya kugombea urais kwa tiketi ya chama cha Demkorasia na Maendeleo ambayo itampa ridhaa ya kugombea urais kupitia umoja wa Katiba ya wananchiukawa unaundwa na vyama vinne vya siasa nchini Tanzania ambavyo ni Chadema, NCCR-Mageuzi, Cuf na NLD.

Aidha, Lowassa aliyekabidhiwa fomu na Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe katika ofisi za Chadema makao makuu yaliyopo Kinondoni jijini Dar es salaam

jana,alichangiwa kiasi kadhaacha pesa kitakachomsaidia katika yake ya matumaini iliyofufukia Ukawa. Katika hafla hiyo  Lowassa aliongozana na Mkewe pamoja na wana familia na ndugu wengine mbalimbali.Mwanasheria mkuu wa Chadema Tundu Lissu alisema kwamba  ili mgombea ameweze kuwania urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ni lazima awe mwanachama wa chama chochote cha Siasa nchini Tanzania, hivyo Lowassa ni mwanachama halali wa Chadema pia amechaguliwa na vikao mbalimbali vya kamati kuu ya chama hicho iliyoketi hadi usiku wa manane.

Uamuzi wa Lowassa kugombea Urais ulipokelewa kwa shangwe na umati wa wananchi uliohudhuria hafla hiyo makao makuu ya Chadema kinondoni jijini Dar es salaam.Mwanasiasa huyo Mkongwe atapambana  na Mgombea kutoka chama cha Mapinduzi Dk.John Magufuli katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu utakaokuwa wa aina yake  mwaka huu wa 2015

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: