ads

STAA wa filamu Bongo, Adam Haji ‘Baba Haji’ juzikati aliangusha sebene la nguvu kwenye Viwanja vya Ngome Kongwe, Zanzibar baada ya kupata taarifa kuwa staa wa kike nchini aliyekuwa akiwania nafasi ya ubunge wa viti maalum mkoani Singida kwa ‘leseni’ ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wema Isaac Sepetu ameangushwa.Akionekana mwenye furaha huku akiserebuka muziki alisema kuwa mbungewenu amekosa ubunge, jambo lililowafanya baadhi ya wasanii wenzake waangue kicheko kwa kuwa inafahamika kuwa ana bifu naye.“Jamani mmesikia majibu? Mbunge wenukashika nafasi ya mwisho, ngoja mimi niendelee kucheza sebene langu,” alisikika Baba Haji huku akiangua kicheko.Bifu la Baba Haji na Wema lilianza kitambo ambapo wawili hao walikutana kwenye Ukumbi wa Bilicanas, Posta jijini Dar ambapo Wema alimchana jamaa huyo kuwa ananuka jasho.

Chanzo: GPL

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: