Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema hali ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kwa sasa imezidi kuimarika na kudai kuwa atasafirishwa kwa matibabu ya awamu ya tatu nje ya Kenya lakini hawatataja ni nchi gani.


Mbowe amesema hayo jana alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kwenye ofisi za Makao Makuu ya chama hicho, wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya Tundu Lissu na kusema mpaka sasa Mbunge huyo anaendelea vizuri na kudai amefanyiwa upasuaji mara 17.

"Tundu Lissu mpaka sasa amefanyiwa upasuaji mara 17 amewekewa damu nyingi kuliko mgonjwa yoyote katika hospitali ya Nairobi kwa miaka 20 iliyopita, lakini Mungu ameendelea kutenda miujiza kwake, mashine zote zilizokuwa zinamsaidia kupumua zimeondolewa, saizi ana pumua bila mashine, mirija yote aliyokuwa anatumia kwa ajili ya chakula imeondolewa na juzi kwa mara ya kwanza aliweza kukaa" alisema Mbowe

Mbowe ameendelea kueleza kuwa "Matibabu ya awamu ya tatu ya Tundu Lissu yatafanyika nje ya nchi haitakuwa tena Kenya wala Tanzania, lakini kwa sababu za usalama hatuwezi kusema atakwenda sehemu gani au nchi gani, ukifika wakati sahihi tutasema hiyo awamu ya tatu ya matibabu itakuwa ya muda mrefu kidogo" amesema Mbowe
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: