
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
Rais Mstaafu wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete amesema uchangishaji fedha kwa ajili ya miundombinu na kilimo ni lazima uende kwa pamoja kwa sababu masuala hayo ni masuala mtambuka kwa maendeleo ya taifa lolote duniani.
Dk. Kikwete amesema hayo jana wakati akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa jijini New York, nchini Marekani, baada ya kushiriki kikao cha ngazi ya juu cha Wiki ya Afrika ambapo masuala ya tabia nchi, miundombinu, kilimo na vijana yamejadiliwa.
Dk. Kikwete amesema uchangishaji usiotosheleza wa fedha katika sekta ya kilimo unakwamisha wakulima kushiriki kilimo cha kisasa kwa kutumia mbegu zisizo na ubora na kusababisha wakulima kukosa mavuno yenye tija.
"Ukiendeleza kilimo unasaidia watu wengi sana na umasikini wa Afrika una sura ya vijijini kwamba masikini wengi waliopo Afrika wapo vijijini na tatizo kubwa la kilimo ni kwamba tunatumia dhana za zamani jembe la mkono linatumika zaidi kuliko mashine na mitambo, asilimia 4 tu ya kilimo chetu tunatumia umwagiliaji na mvua ya mwenyezi Mungu, tatu kilimo chetu hatutumii mbegu bora tunatumia mbegu za asili ambazo hazizalishi sana" alisema Jakaya Kikwete
Post A Comment: