ads

Muigizaji anayesadikika kuwa ni pendwa wa kiume hapa nchini Tanzania, Gabo Zigamba amekanusha tetesi zinazoendelea kuhusu kuwa na uhusiano wa kimapenzi baina yake yeye na Muigizaji Wema Sepetu walipokuwa wakitengeneza filamu mpya ya Kisogo.


Akiwa jana kwenye kipindi cha FNL cha EATV, Gabo aliweka wazi kuwa maneno ya kuzushiwa kati yake na malkia huyo wa filamu yalianza tu baada ya picha za wawili hao kuanza kusambaa ambazo zilikuwa zina mahadhi ya mapenzi na kuwejka wazi kuwa zilikuwa zimebeba maudhui ya filamu.

"Mimi na Wema ni kazi tu. Hakuna kitu cha tofauti ambacho tulikifanya au tulikianzisha tukiwa location kwa sababu mpenzi wake alikuwa anakuja nae mara zote ambazo tulikuwa tuna shoot. 

vipande vyote alikuwa na sisi bega kwa bega sasa hata kama ni hayo mahusiano tungeyaanzisha muda gani? Watu wasifikiri tofauti kwani ukaribu wangu na Wema Sepetu umezalisha filamu ya Kisogo ambayo tunaamini watanzania wataifurahia" alisema Gabo
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: