ads
MAMIA ya wakazi wa viunga vya Jiji la Dar, leo wamejitokeza tena katika usaili wa Shindano la Bongo Star Search ‘BSS’ lililoanza kufanyika jana katika Ufukwe wa Coco jijini humo.
Hata hivyo, baadhi ya washiriki wameonekana kumhofia jaji Salama Jabri kutokana na maneno yake kwenye usaili.
GPL iliweza kuzungumza na Salama kuhusu hofu hiyo hasa baada ya mshiriki mmoja kuzimia kutokana na kukosa nafasi ya kuendelea na shindano.
“Wafanye kazi wasinihofie mimi, niko kazini na wao waje kazini wajitume waoneshe uwezo,” alisema Salama.
Vilevile Jaji Joachim Kimaro ‘Master Jay’ alisema: “Wasanii wa Hip Hop wajipange kwani kuna washiriki wazuri sana wa muziki huo.”Shindano hilo limedhaminiwa na Salama Kondom, Huawei na Kampuni ya Coca Cola.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: