ads

Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) limemfungia mwanamuziki Zuwena Mohamed ‘Shilole” kutojihusisha na kazi yoyote ya sanaa kwa muda wa mwaka mmoja kutokana na kukiuka sheria na maadili.Barua ya  BASATA  imesomeka  hivi“Tarehe 9 May 2015 ukiwa katika onyesho lako la muziki Ubelgiji ulicheza uchi mbele ya hadhira ya wapenda sanaa za Tanzania hivyo kudhalilisha utu wako na jamii ya kitanzania kimaadili”.“BASATA ilipata habari zako, kumbuka pia October 2013 BASATA lilikuonya na ukakiri kwa kuomba msamaha tabia yako ya kucheza bila kuzingatia maadili uwapo jukwaani, BASATA ilikupa nafasi ya kutoa maelezo kwanini usichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kitendo chako lakini umekaidi kutoa maelezo yako”."Baraza limejiridhisha kwamba ulikiuka maadili ya kazi ya sanaa kwenye onyesho lako huko Ubelgiji makusudi na umekiuka sheriakwenye ibara ya 30 (2) ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa kuvunja maadili ya jamii ya Mtanzania hivyo baraza linakusimamisha kujishughulisha na kazi za sanaa nchini na nje ya nchi kwa mwaka mmoja, kufanya kinyume na hayo kutapelekea kupewa adhabu zaidi pamoja na yeyote utakaeshirikiana nae”.

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: